Thursday, 27 December 2018

"MIC IPO TEGETA MDOMO UPO BUZA" Nash mc zuzu

Msanii wa hiphop kutoka Kinasa Nash mc zuzu kupitia ukurasa wake wa Instagram hakuweza kuficha hisia zake kwa wasanii wanaopiga playback wakitumbiza kwenye mashoo.

@maalimnash. Kuelekea Mwaka 2019 Ndugu wasanii jitahidini kupunguza kuigiza kufanya "SHOW" mana asilimia 99.9 ya Wasanii wengi hamfanyi SHOW badala yake mnaigiza, Tabia ya kuendelea kufanya "PLAYBACK" Yani kugandamizia maneno ya wimbo wako ukiwa jukwaani hilo suala halihusiani na SHOW, hilo ni igizo. Mic ipo Tegeta mdomo upo Buza, halafu unaruka ruka saaaaaana, Kesho yake mnaanza kusifiana Flani alifunika sana, kwa kuwa wote mnafanya upumbavu mmoja. Ukuaji wa muziki unaendana na viwango vya Wasanii katika ufanyaji wa maonesho ya Jukwaani. Kwa upande wangu kama wimbo sijaukariri siupigi jukwaani hata mashabiki wauombe kwa kiasi gani.

Huwezi kufunika kwa PLAYBACK katika hadhira ya wanaotambua maana halisi ya muziki, hata kama wewe ni maarufu kiasi gani kama unafanya maigizo ya aina hii achana nayo. 
Najua wasanii wengi hawafanyi mazoezi,walevi, sigara na Bangi nyingi,wanalala mchana, 2019 jiwekeeni ratiba ya mazoezi hata mara 2 kwa juma, wenyewe mnasema Wabongo hawajui hizo hawataki vitu Siriaz sana, lakini wapo Wabongo wengi wanaotaka hivyo vitu Siriaz. 
Katika Hip Hop, Emcee anatakiwa apige SHOW na Mdundo wake na sio agandamizie juu ya wimbo wake, kama sio na Band basi DJ atakuwepo kuhakikisha anamuwekea midundo yake, hata Wasanii mnaoimba pia mnatakiwa kutengeneza vizuri SHOW zenu maana mnagandamizia na bado mnakata pumzi. 
PLAYBACK SIO MZUKA HIZO NI SHOW ZA WANYONGE. 
Naitwa Nash Mc Maalim.

No comments:

Post a Comment