Saturday, 22 December 2018

MO'' KUILETA NDINGA MPYA TZ

''MO'' KUILETA NDINGA MPYA TZ


Siku Zinapozidi kusogea hukipata kupishana na hii gari hapa town basi ujue tajiri kijana kutoka Tanzania na boss wa timu ya Simba sc anapita. Mo amesibitisha Hilo kupitia kwenye account yake instagram baada ya kupost picha ikiwa ndani ya gari hiyo kali ya kifahari ambayo hakuna mtu yoyote Tanzania anamiliki na kuandika caption inayosomeka hivi '' time for something new''.

Gari hiyo aina ya Tesla Model 3 ni gari lisilo na injini. Linatumia umeme. Halina muungurumo. Lina camera za dashboard, yaani dashcam. Ni kamera za mzunguko wa nyuzi 360 na huchukua video zenye ubora wa hali ya juu, yaani HD.

Tesla Model 3 ni gari lisilo na injini. Linatumia umeme. Halina muungurumo. Lina camera za dashboard, yaani dashcam. Ni kamera za mzunguko wa nyuzi 360 na huchukua video zenye ubora wa hali ya juu, yaani HD.

Tesla Model 3 halina ufunguo, linatumia rimoti. Ukishaingia kwenye gari, kwenye dashboard kuna kitu mfano wa tablet. Hiyo ndiyo unaitumia kuendeshea gari
Hata rimoti yake si muhimu sana. Unaweza kuweka App ya gari kwenye simu, kisha utaitumia simu yako kuendesha gari, kufungua milango, kufunga na kulidhibiti.

Tesla Model 3 lina mfumo wa autopilot ya kiwango cha juu kama ndege. Autopilot huwezesha ndege kujiongoza yenyewe ikiwa angani.

Kwa Tesla Model 3 kuwa na autopilot, inalifanya gari hilo kujiendesha lenyewe. Lina kamera zenye kuona mbali (autopilot cameras), dereva akilikimbiza, lenyewe hutambua hali halisi ya barabara, kwa hiyo hupiga alarm. Dereva asipotii, gari lenyewe hufunga breki. Gari lina automatic break.

No comments:

Post a Comment